Sunday 16 August 2020

Tetesi za Soka Ulaya 16.08.202

 https://ichef.bbci.co.uk/news/800/cpsprodpb/CC46/production/_113949225_saul_getty.jpg

Manchester United iko tayari kutoa ofa kwa kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 25, anayesemekana kuwa thamani yake ni pauni milioni 70 ya mkataba wa muda mrefu wa pauni 150,000 kwa wiki ili kumsajili mchezaji huyo kutoka Atletico Madrid msimu huu. (Star)

 Wakati huohuo, Manchester United inafikiria makubaliano ya mabadilishano ambapo kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, atarejea Juventus huku mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 26, akihamia kwao. (Tuttosport - in Italian) 

Matumaini ya Chelsea kumsajili mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak, 27, yameimarika huku klabu ya La Liga ikisemekana kuwa makini kutafuta mbadala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovenia. (Football London) 

 Kocha wa Barcelona Quique Setien huenda akapigwa kalama baada ya kuchabangwa mabao 8-2 katika Ligi ya Mabingwa na Bayern Munich Ijumaa - na Mauricio Pochettino, Xavi na Ronald Koeman ndio walio kifua mbele katika orodha ya atakayemrithi Setien huko Nou Camp. (Mundo Deportivo, in Spanish) 

 Taarifa za Uhispania zinadai kwamba aliyekuwa kocha wa Tottenham na Southampton Pochettino tayari alishafanya mazungumzo na Barcelona siku nyingi tu kabla ya timu hiyo kuvuliwa nguo Ijumaa. (Express) Blues huenda ikamtoa mlinga lango wao Kepa Arrizabalaga kwa Atletico kama sehemu ya mabadilishano kwasababu haiko tayari kutimiza bei ya klabu hiyo ya Uhispania ya pauni milioni 110 ili kuwa na mchezaji Oblak. (Star)

No comments:

Post a Comment