Thursday 20 August 2020

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 20.08.2020


 José Mourinho anataka kumrejesha Tottenham mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 31. (Cuatro-in Spanish). Beki wa kati wa Paris St -Germain Thiago Silva, 35, ambaye anaondoka kwenye klabu hiyo ya Ufaransa baada ya fainali za michuano ya klabu bingwa Ulaya amepewa ofa na Chelsea (Telegraph). Kushindwa kufikiwa kwa maelewano binafsi ya mkataba wa Muingereza Jadon Sancho, 20 kumeongeza ugumu wa uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United (ESPN).

Manchester United wanaweza kuipatia Aston Villa mlinda mlango Sergio Romero,33, kama sehemu ya makubaliano ili kumpata kiungo wa kati Jack Grealish, 24. (Mail). Chelsea na Atletico Madrid wana mpango wa kumpata winga Federico Bernardeschi, 26, anayekipiga Juventus. ( Calciomercato-in Italian).

Liverpool inajiandaa kumuuza kiungo Marko Grujic, 24, na winga Harry Wilson, 23, msimu huu (Mirror).

Chelsea watakamilisha kumsajili kiungo wa kati wa Kijerumani Kai Havertz, 21, wiki hii kwa mkataba wa miaka mitano iwapo wao na Bayer Leverkusen wanaweza kupunguza tofauti ya pauni milioni 18 ya thamani ya mchezaji huyo. (Telegraph).

Kiungo wa kati wa Manchester United Mbrazili Andreas Pereira, 24, analengwa na Benfica na Valencia. (ESPN). United imerejesha shauku yao kwa beki wa kushoto Alex Sandro, 29, anayeichezea Juventus ( Calciomercato-in Italian).

Cottagers wameingia pia katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Muigereza Callum Wilson, 28. (Telegraph).

Leeds inatayarisha kitita cha pauni milioni 10 kwa ajili ya winga wa Rangers, Ryan Kent, 23. (Sun).

Kocha wa zamani wa England Sven Goran Eriksson anajiandaa kuwa kocha mpya wa Jamaica. ( Mirror).

Chelsea itafanya mazungumzo na kiungo wa kati Conor Gallagher huku Newcastle na Crystal Palace zote zikionesha nia ya kumsajili msimu uliopita .

No comments:

Post a Comment