Tuesday 18 August 2020

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 18.08.2020

 Manchester City imefufua tena azma yake ya kutaka kumsajili mlinzi wa Napoli raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 29, baada ya kubanduliwa kwenye Ligi ya Mabigwa. (La Repubblica via Talksport)

Mkurugenzi Mtendaji wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke anadai klabu hiyo haiko chini ya shinikizo lolote la kumuuza mlengwa wa Manchester United Jadon Sancho, 20, licha ya mahesabu kuonesha hasara ya pauni milioni 39.8 kwa kipindi cha mwaka hadi 30 Juni 2020. (Manchester Evening News)

Arsenal imeanzisha mchakato rasmi wa mkataba mpya wa miaka mitatu wa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang wenye thamani wa zaidi ya pauni 250,000-kwa wiki. (Mail)

Manchester United inamfuatilia kwa karibu winga wa Brazil na Juventus, 29, Douglas Costa inapoanza safari yake ya usajili wa msimu. (Sky Sports)

Liverpool bado ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara lakini imeiarifu klabu hiyo ya Bundesliga kuwa haiko tayari kulipa pauni milioni 27.2 kwa raia huyo wa Uhispania, 29, ambaye mkataba wake umesalia na mwaka mmoja. (Guardian)

Klabu ya Benfica ya Ureno inaonekana kuiongoza Leeds United katika kinyang'anyiro cha kumsajili nyota wa Paris St-Germain raia wa Uruguay Edison Cavani huku mchezaji huyo, 33, akiwa anapatikana kwa uhamisho wa bure. (Goal)

West Brom na West Ham wamearifiwa kwamba kitita cha karibu pauni milioni 2.7 kitahitajika kumsajili beki wa Istanbul Basaksehir na Brazil Junior Caiçara, 31. (Sport Witness via Birmingham Mail)

Inasemekana kwamba Juventus haina tena msimamo wa kwamba Cristiano Ronaldo hawezi kuhamishwa hadi timu nyingine na huenda ikaamua kumuuza mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 54 huku Paris St-Germain ikimfuatilia kwa karibu kutaka kumsajili mchezaji huyo, 35. (Sport)

Barcelona iko tayari kuanzisha jaribio la kumsajili tena Neymar kutoka Paris St-Germain wakati inapokuwa mbioni kujikwamua baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa. (Mail)

No comments:

Post a Comment