Saturday 22 August 2020

Tetesi za soka Ulaya


 Kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman anataka kumleta kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 29, Nou Camp. (Algemeen Dagblad, via Express)

Beki wa kati wa Lille na Brazil Gabriel Magalhaes, 22, amechelewa kufanya maamuzi ya mwisho ya kuelekea Arsenal baada ya Manchester United kuonekana kuwa na uwezekano wa kutoa kitita fulani kwa ajili yake. (Telegraph)

Manchester United imeonesha kunyamaza juu ya mpango wake wa makubaliano ya mkopo kwa winga wa Juventus na Mbrazil Douglas Costa, 29, na badala yake inafikiria kumsajili winga wa Bournemouth na Wales David Brooks, 23. (Manchester Evening News)

United imearifiwa kwamba ni lazima ilipe Bournemouth pauni milioni 40 kumsajili Brooks. (Sun)

Paris St-Germain inamnyatia beki wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot, 21. (O Jogo - in Portuguese)

Beki wa kati wa Manchester United Chris Smalling, 30, anafuatilia kwa karibu makubaliano ya mkopo na Roma baada ya msimu uliopita kuwa Serie A. (La Gazzetta dello Sport, via Mirror)

Mazungumzo mapya ya mkataba kati ya United mlinda lango Mwingereza Dean Henderson, 23, yako katika hatua za mwisho. Makubaliano yao yanasemekana kuwa na thamani ya zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki. (Sky Sports)


No comments:

Post a Comment