Monday 5 October 2020

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA NA 10 WAJERUHIWA.

 


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam,

Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali iliyopelekea watu watano kupoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwa

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi katika eneo la Chang'ombe na imehusisha daladala inayofanya safari kati ya Temeke na Muhimbili na lori la mchanga

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe

amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa daladala, ambapo dereva amekimbia na Polisi inaendelea kumtafuta.

No comments:

Post a Comment