Thursday 22 October 2015

RAISI KIKWETE ASEMA NENO KUHUSU UCHAGUZI


   Zikiwa zimebaki siku mbili pekee kuingia katika kufanya maamuzi sahihi na yenye maslahi kwa Taifa zima  la Tanzania katika kufanya uteuzi wa  ngazi mbalimbali za uongozi ikiwemo ya udiwani ,ubunge na mrithi wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania .anayemaliza muda wake Dr Jakaya Kikwete amewahakikishia watanzania uchaguzi utakuwa huru na wa amani na wasiwe na hofu, na kuwaonya wale ambao wanapanga kuleta fujo watakiona.


                                      Raisi wa Tanzania Mh.Dk.Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Kikwete ambaye pia ni mweyekiti wa CCM ametoa tahadhari hiyo hapa Chakechake Pemba wakati akiwahutubia umati wa wanachama wa CCM na wananchi waliofika katika uwanja wa Gombani ya kale katika mkutano wa mwisho kwa Pemba wa kampeni ya mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya CCM ambapo amesema yeye bado ni amiri jeshi mkuu wa nchi na kuwataka watanzania kwenda kwa wingi kupiga kura.

No comments:

Post a Comment