Kikosi cha ALgeria (The Desert worriors)
Msafara wa timu ya Taifa ya Algeria (The Desert Warriors) unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamis kwa ndege binafsi ya kukodi, ukiwa na jumla ya watu 65 wakiwamo wachezaji 24 tayari kwa mchezo wa Jumamosi Novemba 14 dhidi ya wenyeji Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kocha mkuu wa timu hiyo Iitakayofikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Kempsinki, Christian Gourcuff raia wa Ufaransa ametaja kikosi cha wachezaji 24, wakiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya kwa ajili ya kuikabili Tanzania.
Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili Alhamisi ni walinda mlango, Doukha Izeddine (JS Kabliye), M’bolhi Rais (Antalyaspor), Asselah Malik (CR Belouizdad), walinzi Zeffane Mehdi (Rennes), Medjani Carl (Trabzonspor), Ziti Mohamed (JS Kabliye), Mesbah Eddine (Sampordia), Bensebaini Ramy (Montpeller), Belkarou Hichem (Club African), Ghoulam Faouzi (Namples), Mandi Aissa (Reims).
Viungo ni Guedioura Adlane (Watford), Boudebouz Ryad (Montpeller), Taider Saphir (Bologna), Abeid Mehdi (Panathinacos), Bentaleb Nabil (Tottenham), Ghezzal Rachid (Lyon), Melsoub Walid (Lorient), Marhez Ryad (Leicester).
Washambuliaji Benrhama Said (Nice), Sliman Islam (Sporting Lisbon), Belfodil Ishak (Beni Yas), Brahimi Yassine (FC Porto) na Bounedjah Baghdad (Etoile du Saleh)
No comments:
Post a Comment