Tuesday 10 November 2015

Rais wa nigeria amfuta kazi mkuu wa Taasisi ya kupambana na Rushwa


          Rais wa Nigeria Mahammudu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amemfuta kazi mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini humo.
Hata hivyo bado hajaeleza sababu zilizomfanya kumpiga kalamu Ibrahim Lamorde ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu 2011.
Rais Buhari alishinda kiti cha Urais nchini humo, katika uchaguzi uliofanyika mwaka huu.
Baraza lake la mawaziri linatarajiwa kuapishwa baadaye wiki hii, zaidi ya miezi mitano baada ya kuingia madarakani.

No comments:

Post a Comment