Monday, 21 December 2015

Arsenal na Manchester City zatunishiana misuli usiku huu

 Arsenal vs Man City LIVE score EPL: Follow the Emirates Stadium action









Arsenal na Manchester City zapambana katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England usiku huu katika uwanja wa nyumbani wa Arsenal, Emirates timu zote mbili zikiwania ushindi kujaribu kubanana na vinara Leicester City.
 
Arsenal wanashika nafasi ya pili nyuma ya Leicester yenye points 38 huku Arsenal wakiwa na points 33 wakati City wakiwa na points 32. Hivyo ushindi wowote kati ya timu zote mbili ni muhimu kuikaribia Leicester ambao wanaongoza ligi wakiwa wamepoteza mechi moja tu tangu kuanza kwa msimu.
 

Sergio Aguero ni mchezaji muhimu katika kikosi cha City, ambapo msimu uliopita alitwaa kiatu cha dhahabu kama mfungaji bora wa ligi. Uwezo wake wa upachikaji mabao unamfanya kuwa moja ya washambuliaji tishio zaidi ulimwenguni.

Arsenal kwa upande wao bado wamekua na wimbi kubwa la majeruhi huku mshambuliaji wao hatari Alexis Sanchez akiwa nusu kwa nusu kucheza mechi ya leo baada ya kuwa majeruhi tangu wiki iliyopita. Wachezaji wengine muhimu ambao ni majeruhi ni pamoja na kiungo mkabaji Coquelin.

Arsenal vs Manchester City: Which side is best placed to win Premier League?

No comments:

Post a Comment