Kocha wa Rayo Vallecano Paco Jemez amesema kuwa timu yake imedhalilishwa na kuteswa kwa kufungwa 10-2 na Real Madrid hapo jana.
Jemez anahoji kuwa ligi ya Uhispania imepoteza hadhi yake kufuatia matokeo ya aina hiyo.
Hii hainufaishi Madrid, sisi au soka ya Uhispania.
Tumepoteza hadhi. ," alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 45.
"Leo hakuna aliyeshinda, sote tumepoza. Ni aibu, aibu kubwa.’’
''Haya ndio mambo yanayotokea na ninatumai kuwa hatutayaona yakitokea tena kwingine."
Hata hivyo Cristiano Ronaldo alikuwa na mechi tulivu ambapo alijipa goli moja kila kipindi.
Licha ya Kutangulia kwa uongozi wa mapema wa 2-1 , walizabwa na Real baada ya wachazaji wake wawili kupewa kadi nyekundu.
Jemez aliongeza kuwa "Ni kitambo sana tangu nishuhudia jambo lisiloaminika na la aibu.
"Hisia yangu kuu ni kuwamotisha wachezaji wangu waliojitolea leo.
Ni ngumu kuwatuliza kwa sababu wanahisi kudhalilishwa na kuporomoshwa.
" "Sina la ziada, anayetaka kunielewa, ataelewa.
"Idadi kubwa ya watu hapa hawakufarahia walichoona- ni vipi jambo kama hili linaweza kutokea katika ‘ligi bora duniani? Haipaswi kutokea popote.
"Kulikuwa na wakati ilionekana si sawa. Na unapoona wachezaji wakitokwa na machozi, sio kwa sabau tumelazwa mabao 10 lakini kwa kilichotokea."
Kocha wa Real Madrid, Rafa Benitez amemjibu Jemez kwa kusema: "Kuna mechi nyingi ambapo tumekumbwa na hali zisizotupendelea ambayo haikutunufaisha sisi.
"Sikusema lolote wakati huo na sasa pia sitasema. Kama kocha ninastahili kuifanya timu ifunge magoli na icheze vizuri. Tutaendelea hivyo
No comments:
Post a Comment