Zaidi ya wakoaji 1000 wanatafuta watu walionusurika kusini mwa China siku moja baada ya maporomoko ya ardhi
kuangusha nyumba 33 katika mji wa Shenzhen .
Watu saba wameokolewa
lakini wengine 85 bado hawajulikani waliko baada ya tope kuporomoka
katika mtaa mmoja wa kiviwanda katika mji wa Shenzhen.Takriban watu 900 walihamishwa kabla ya kutokea kwa maporomoko hayo.
Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa udongo huo ulikuwa umejazwa eneo moja kinyume cha sheria.
Udongo huo unatokana na timbo inayotumika kusaga mawe ya ujenzi na pia jaa ya mabaki ya ujenzi.
Mji wa Shenzhen ni moja kati ya miji mikubwa zaidi nchini China mbali na kuwa mji mkubwa zaidi kiviwanda.
Poromoko hilo la ardhi liliathiri takriban mita laki nne mraba likifunika ardhi na mita 10 ya udongo.
Shirika la habari la taifa Xinhua limesema maporomoko hayo yalisababisha mlipuko katika kituo kimoja cha mfereji wa gesi ya kupikia.
Takriban mita mia 400 ya mifereji ya gesi imeharibiwa.
No comments:
Post a Comment