CHAMA cha Mapinduzi mkoani
Lindi kimetetea jimbo lake la Masasi katika uchaguzi ulifanyika Jana baada ya
kuahirishwa Oktoba 25 Mwaka huu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mgombea ubunge
wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha NLD, Dokta Emamanuel Makaidi kufariki Dunia
Kwa mujibu wa matokeo ya
uchaguzi huo yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jimbo la Masasi, Fortunatus
Kagoro amesema kuwa Bwana Rashid Chuachua amepata kura 16,597 akifuatiwa na
Ismail Makombe Maarufu kama Kundambanda wa CUF, aliyepata kura 14,019.
Wengine Walioshiriki katika
Uchaguzi huo ni Swaleh Ahmad wa CHADEMA, aliyepata kura 512, Omary Timothy wa
ACT-Wazalendo Aliyepata kura 347, na Angelus Thomas wa NLD Aliyepata kura 70.
No comments:
Post a Comment