KATIBU tawala wa mkoa wa Shinyanga,
Abdul Dachi, ameziagiza Halmashauri zote sita za mkoani humo kutenga bajeti ya
lishe ya kkatika mwaka wa fedha 2016/17 kwa lengo la kuondoa tatizo la
utapiamlo kwa watoto
Takwimu zinaonyesha mkoa huo
ni miongoni mwa mikoa nchini, inayokabiliwa na asilimia kubwa ya watoto wenye
utapiamlo na udumavu na kusababisha kuzalisha kizazi cha watu wenye afya
mgogoro na kushindwa kujenga taifa lao.
Dachi ametoa agizo hilo
wakati akifungua kikao cha wadau wa afya mkoani Shinyanga, kilichoandaliwa na
shirika la Save the children kwa madhumuni ya kutoa taarifa ya mradi wa ANI na
kupanga mikakati mipya ya kutokomeza tatizo la utapiamlo kwa watoto
Naye afisa lishe mkoa,
Mariamu Mwita, amesema takwimu za utapiamlo mkoani humo ni asilimia 43 kwa
watoto wadumavu, 75 wakiwa na upungufu wa samu, madini chuma asilimia 48,
vitamin A 37, waliokonda 3 na uzito pungufu 10.
Kwa upande wake afisa mradi
wa kupambana na utapiamlo mkoani Shinyanga toka shirika hilo, Augustino
Mwashiga, amesema mradi huo wa Accelerating nutrion improvement Ani, umefanyika
kwa miaka miwili 2014/15 uliokuwa na lengo la kuhamasisha jamii kufuata sheria
za lishe bora.
No comments:
Post a Comment