KLABU
ya Arsenal imeanza mazungumzo na FC Basel ya Uswisi kwa ajili ya kutaka
kumsajili kiungo wao Mohamed Elneny.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Misri mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na klabu hiyo
mwaka 2013 na kufanikiwa kushinda mataji ya Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa misimu
mitatu
Elneny
anakadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni tano, ingawa atahitaji kibali cha
kufanyia kazi nchini Uingereza. Kama Arsenal wakifanikiwa kumsajili
wanaweza kumtumia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwani Basel
Mohamed Elneny
Hawakufanikiwa kufuzu hatua ya makundi msimu huu.
Meneja
wa Arsenal Arsene Wenger anajaribu kuongeza nguvu safu yake ya kiungo baada ya
Francis Coquelin na Santi Cazorla kupata majeruhi ya muda mrefu huku Aaron
Ramsey na Mikel Arteta nao wakikosa michezo kadhaa kutokana na majeruhi.
No comments:
Post a Comment