KLABU ya
Manchester City inadaiwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kumng’oa
Lionel Messi kutoka Barcelona.
Taarifa za
gazeti la Sport zimedai wawakilishi wa Messi wamemuahidi kuwa atavuna kiasi cha
paundi milioni 20 kwa msimu kama akitua City kiasi ambacho kinazidi kile
anachopewa na mabingwa hao wa Hispania.
Wakati
Barcelona wakiwa hawana mpango wa kufanya mazungumzo ya mkataba mpya mpaka
msimu ujao, klabu hiyo ina uhakika Messi ataikacha ofa hiyo kama alivyofanya
wakati alipofuatwa na Paris Saint-Germain na Chelsea huko nyuma. Kwasasa
City hawataweza rasmi ofa yao kwa Barcelona mpaka watakapoona dalili kwa Messi
kuwa yuko tayari kukubali ofa yao.
No comments:
Post a Comment