Tuesday 29 December 2015

MESSI ASHINDA TUZO ZA GLOBAL SOCCER




KLABU ya Barcelona na nyota wa Lionel Messi wameibuka washindi tena katika tuzo za Globe Soccer zilizofanyika huko Dubai jana, kwa kuondoka na zawadi ya timu na mchezaji bora. 

Messi alisafiri kutoka Argentina kwenda kuhudhuria sherehe hizo. Akihojiwa Messi amesema ni jambo zuri kupokea tuzo hiyo lakini kama asemavyo siku zote timu nzima ndio inafanya hilo kuwezekana. 
 

Barcelona imefanikiwa kushinda mataji matano mwaka 2015 ambayo ni La Liga, Kombe la Mfalme, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Super Cup ya Ulaya na Klabu Bingwa ya Dunia. Taji pekee ambalo wamelikosa kwa mwaka huu ni Super Cup ya Hispania ambalo lilikwenda kwa Athletic Bilbao. 

Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Marc Wilmots ametajwa kama kocha bora wa mwaka huku Benfica ya Ureno wao wakichukua tuzo ya kuwa na shule bora ya soka. Viungo Andres Pirlo wa Italia na Frank Lampard wa Uingereza wao wamepewa tuzo kutokana na kucheza soka kwa kipindi kirefu zaidi

Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 - Lionel Messi

Klabu Bora 2015 - Barcelona

Rais Bora 2015 - Josep Maria Bartomeu

Mvuto kwenye Vyombo vya Habari - Barcelona

Tuzo ya Mchezaji Mkongwe- Frank Lampard

Tuzo ya Mchezaji Mkongwe - Andrea Pirlo

Wakala Bora 2015  - Jorge Mendes

Kocha Bora 2015 -  Marc Wilmots

Akademi Bora 2015 - Benfica

Mchezaji Bora wa GCC 2015 - Yasir Al-Shahrani

Refa Bora 2015 - Ravshan Irmatov

No comments:

Post a Comment