MCHEZAJI wa
zamani wa kimataifa wa El Salvador, Alfredo Pacheco ameuawa kwa kupigwa
risasi. Mtu mwenye silaha anadaiwa kumfuata Pacheco mwenye umri wa miaka
33 na kumfyatulia risasi kadhaa katika kituo cha mafuta kilichopo mji wa Santa
Ana kilometa 76 kutoka magharibi mwa mji mkuu wa San Salvador.
Maofisa
wa polisi wamesema watu wengine wawili walijeruhiwa katika tukio hilo ambalo
bado wanafanya uchunguzi wa chanzo chake.
Beki
huyo ambaye ndio mchezaji wa aliyeichezea mechi nyingi zaidi nchi yake,
alifungiwa maisha kujishughulisha na masuala ya soka mwaka 2013 baada ya
kukutwa na hatia ya kupanga matokeo.
Pacheco
na wachezaji wengine 13 wa timu ya taifa walikutwa na hatia ya kupkea rushwa na
kupanga matokeo katika mechi kadhaa kati ya mwaka 2010 hadi 2013.
El Salvador, ni Taifa ndogo lililoko Amerika ya
Kati, ni moja ya mataifa yenye viwango vya juu zaidi vya mauaji.Mapema mwezi huu, mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta, 26, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa likizoni katika mji wake wa kuzaliwa.
No comments:
Post a Comment