Tuesday, 29 December 2015

MKUTANO wa mawaziri wa mambo ya nje wa Ethiopia, Sudan na Misri, kujadili mradi wa umeme



 
MKUTANO wa mawaziri wa mambo ya nje wa Ethiopia, Sudan na Misri, kujadili mradi wa umeme wa  Ethiopia umemalizika leo mjini Khartoum- Sudan Lengo  kuu  la mkutano huo ni  kuangalia namna ambavyo  mradi wa umeme wa  Ethiopia unavyoathiri nchi za Sudan na Misri katika matumizi ya mto Nile Kwa mara ya kwanza Jumamosi hii  Ethiopia ilijaribu kubadilisha muelekeo wa mto  Nile  ili  kupita katika mabwawa hayo, baada ya kukamilika njia  ya kwanza ya maji ya  kuzalishia umeme .Awali  mwezi march  mwaka huu, Sudan, Misri na Ethiopia ziliweka makubaliano mjini Khartoum Sudan  ya kusini   kuiruhusu Ethiopia kuendelea na Ujenzi wa mradi wa umeme.




No comments:

Post a Comment