MTU mmoja amefariki dunia
na wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari moja linalosadikiwa kubeba mabomu
kuripuka karibu na uwanja wa ndege wa kimataiafa mjini Qaboul-Afghanistan mapema leo.
Duru za ki usalama za
nchi hiyo zinaripoti kuwa gari hilo
lilikuwa limelenga gari la vikosi vya
umoja wa kujihami wa nchi za magharibi NATO
Tukio hilo limekuja sambamba na ujio wa Amiri jeshi mkuu wa Pakistan generali Raheel
sharif kuwasili nchini Afghanistan ili kufanya mazungumzo ya amani na
viongozi wan chi hiyo.
Tukio hilo ni la pili kutokea
ambapo mwezi uliopita jeshi la
Afghanistan liliripoti kuwa watu 37
walipoteza maisha yao na wengine kadhaa kujeruhiwa katika hujuma
iliyopangwa na kundi la Taliban katika
uwanja wa ndege wa kandahari
No comments:
Post a Comment