WAZIRI wa afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amefanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na kukutana na dosari Mbalimbali
Moja ya mambo
yaliyomkera Ummy ni kuwakosa Madaktari wa Zamu katika Hospitali hiyo pamoja na
ukosefu wa Mashuka kwa wagonjwa hali iliyowalazimu kutandika kanga zao.
Ilikuwa ni ziara
ya kustukiza iliyofanywa na waziri wa afya maendeleo ya jamii ,jinsia wazee na
watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ikiwemo Ukosefu wa vitanda
pamoja na madaktari walioajiriwa kutokuwepo.
Mwalimu anatembelea vitengo mbalimbali vya
hospitali hiyo na kukutana na madaktari wanafunzi huku wale Madaktari Waajiriwa
walioko zamu wakiwa hawajulikani walipo
No comments:
Post a Comment