Monday, 21 March 2016

Haya ndio matokeo kamili ya uchaguzi wa marudio zanzibar

Tume ya Uchaguzi ya ZANZIBAR imemtangaza DR, SHEIN kuwa mshindi mara baada ya kukamilika uhesabuji wa kura zote zilizopigwa katika visiwa vya PEMBA na UNGUJA .


DR. ALLY MOHAMED SHEIN ameshinda katika uchaguzi huo kwa kupata kura 299,982 sawa na asilimia 91.4.

Akifuatiwa na HAMAD RASHID MOHAMED mgombea wa chama cha ADC kwa kupata kura 9734 sawa na asiilimia 3 ya kura zote zilizopigwa.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi zanzibar ZEC - JESHA SALIM JECHA amesema kura halali zilizopigwa ni 341,895 sawa na aasilimia 97 na kura zilizoharibika ni 13,538.

Kufuatia matokeo hayo jecha amemtangaza dr. Ally mohamed shein kuwa rais wa zanzibar kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo, na kukabidhiwa hati ya ushindi, Rais Dkt SHEIN amewashukuru wananchi wa zanzibar kwa kumchagua tena, huku akiwaahidi kuendelea kuwatumikia wanachi wote bila kubagua vyama.
Naye mshindi wa nafasi ya pili HAMAD RASHID MOHAMED, amesema ni vyema wananchi wa zanzibar waoneshe ushirikiaano kwa rais aliyeshinda ili waweze kuingia katika uchumi wa kati.

Amesema mchakato wa kisiasa ni kama mfumo wa maisha, hivyo ni vyema wakaacha tofauti zao za kisiasa na kumpa fursa mgombea aliyeshinda kutimiza majukumu yake.

No comments:

Post a Comment