Saturday 23 April 2016

Beki wa Liverpool Mamadou Sakho anachunguzwa na UEFA.

 The Liverpool defender Sakho sprints away in celebration having scored in the Merseyside derby
Beki wa Liverpool Mamadou Sakho anachunguzwa na UEFA kwa kufeli ukaguzi wa madawa ya kulevya.

Ijapokuwa raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 hajapigwa marufuku rasmi, hatashiriki mechi yoyote wakati uchunguzi huo unapoendelea kulingana na Liverpool.
BBC radio 5 inasema kuwa Sakho alipatikana na dawa za kusisimua misuli baada ya mechi ya UEFA kati ya Liverpool dhidi ya Manchester United.
 Mamadou Sakho (centre) looks on from the stands as Liverpool host Newcastle at Anfield on Saturday
  Mamadou Sakho katikati akitazama mchezo wa Liverpool na Newcastle
Sakho aliyesajiliwa kwa pauni milioni 18 kutoka Paris St-Germain mwaka 2013 amecheza mechi 34 msimu huu ikiwemo mechi 10 katika ligi ya Yuropa.
Alifunga katika ushindi wa Liverpool wa 4-3 dhidi ya Borussia Dormund mnamo tarehe 14 mwezi Aprili na kufuzu katika nusu fainali ya kombe hilo.
Liverpool ambayo ni ya 7 katika jedwali la ligi ya Uingereza inaialika Newcastle siku ya Jumamosi.

No comments:

Post a Comment