Sunday, 24 April 2016

Dola milioni 100 kutolewa na Benki ya Dunia Tanzania


Benki ya Dunia (WB) ipo katika mchakato wa kutoa dola za Marekani zaidi ya milioni 100, kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ndani ya hifadhi zote za Taifa, ili ziweze kuingiza watalii zaidi.

Hayo yalisemwa jana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha, Dk. Christopher Timbuka na kueleza kuwa fedha hizo zinazotarajiwa kutolewa na benki ya Dunia ni kwa ajili ya kuendeleza hifadhi mbalimbali zilizopo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Dk. Timbuka aliongeza kuwa baadhi ya watalii wanashindwa kufika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutokana na changamoto ya miundombinu mibovu ya barabara, ambayo ni kikwazo kwa watalii kuingia ndani ya hifadhi hiyo haswa nyakati za mvua.
Naye Mhifadhi Utalii wa Hifadhi hiyo, Tutindaga Mdoe alisema hifadhi hiyo ni miongoni mwa hifadhi kubwa yenye wanyama wa aina mbalimbali na hivi sasa wawekezaji kadhaa wanaomba kuwekeza zaidi katika hifadhi hiyo ambayo inamuonekano mzuri kutokana na kuwa na mito mingi.

No comments:

Post a Comment