Sunday 24 April 2016

Papa wemba afariki Dunia

 
Mwanamuziki mkongwe kutoka Kongo, Papa Wemba amefariki Dunia.
Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba amefariki dunia
Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.
 
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous,
Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.
Msanii huyo nguli mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni anasemekana alianza kutetemeka, kisha akaanguka na kuzirai, alipokuwa akitumbuiza jukwaani Abidjan.
 
Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.
Papa Wemba alijiunga na kikundi maarufu cha Zaiko Langa Langa kilipoanzishwa mwaka wa 1969 mjini Kinshasa.
Wemba wakati huo alijiunga na wanamuziki wenza wa Congo (kama ilivyojulikana wakati huo) Nyoka Longo Jossart, Manuaku Pepe Felly, Evoloko Lay Lay, Bimi Ombale, Teddy Sukami, Zamuangana Enock, Mavuela Simeon, Clan Petrole miongoni mwa wengine.
Wakati huo akianza Papa Wemba , jukwaaa la muziki nchini humo lilikuwa limetawalwa na vigogo wa muziki Franco Luambo wa TPOK Jazz, Tabu Ley Rochereau wa Afrisa, na makundi mengine mapya kama vile Les Grands Maquisards, Le Trio Madjesi, Bella-Bella, Thu Zaina na Empire Bakuba.
Hata hivyo sauti ya kipekee ya Papa Wemba akijulikana wakati huo kwa majina yake kamili Jules Presley Shungu Wembadio ilikonga mioyo ya wapenzi wa Soukus.
Kilele cha ufanisi wa kundi la Zaiko Langa Langa ulikuja miaka ya mapema ya 1973.

 
 Vibao vyake ni kama
Mwasi,show me the way, Yolele, mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) , "Zania" (Mavuela Somo.


No comments:

Post a Comment