Serikali
ya Mkoa wa Lindi imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Lindi, Oliver Vavunge na kumwomba Waziri Mkuu amsimamishe
kazi Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Kilimo cha Umwagiliaji Maji Taifa
kutokana na hasara ya Sh milioni 500 katika mradi wa umwagiliaji maji wa
Kiwalala Narunyu, Lindi.
Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliyasema hayo jana wakati
alipozungumza na wananchi kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Kiwalala
wilayani humo juzi.
Zambi
alisema kati ya fedha zilizowekwa kwa ajili ya kutekeleza mradi wa
umwagiliaji maji ni Sh milioni 700, kati ya hizo Sh milioni 500
zilishatumika na kubakia Sh milioni 200.
Alisema
mradi huo ulioanza mwaka 2011 mpaka mwaka huu haujakamilika na fedha
zilishachukuliwa, na kufafanua kuwa mkurugenzi anaingia hatiani kutokana
kutokuwa makini juu ya mradi huo katika usimamizi.
Alitoa
fedha kwa nyakati tofauti kumlipa mkandarasi wa kwanza na kuvunja
mkataba naye Sh milioni 121, wa pili alivunja na alitoa Sh milioni 226
na Sh milioni 116, mwaka jana.
Zambi
alisema fedha hizo zilikuwa zinachukuliwa baada ya makandarasi wakidai
kwa kazi walizokuwa wakizifanya kwa kuweka miundombinu ya shamba hilo.
Alisema
Tume ya Umwagiliaji Maji nayo wataalamu wake hawakuwajibika ipasavyo
juu ya usimamizi wa mradi huo kwani wao ndiyo waliotia hasara kwa
mamlaka kutokana na barua zao walizokuwa wanaziandika juu ya mradi huo.
Barua
ya kutoka Ofisi ya Kanda ya Kusini Tume ya Umwagiliaji Maji
iliyoandikwa Septemba mwaka jana ilieleza kuwa mradi huo unatekelezeka
kwa kiwango hicho cha fedha, na Novemba 27, mwaka jana, Kaimu Mkurugenzi
wa Umwagiliaji Maji alifika na kuandika barua kuwa mradi huo hauwezi
kutekelezeka, kinachotakiwa ni kufanya tathmini upya.
Alitoa ushauri kujenga banio dogo. Zambi alisema kwa jumla ushauri wao haukuwa mzuri na kusababisha hasara kwa mamlaka husika.
No comments:
Post a Comment