Wednesday, 20 April 2016

Kutoka bungeni Serikali yasema ada elekezi kutoathiri shule binafsi

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi STELLA MANYANYA
Naibu waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi Mhandisi STELLA MANYANYA amesema ada elekezi haitaathiri shule binafsi kwa kuwa ada hizo zitatolewa kulingana na uhalisia wa shule husika.

Akijibu swali bungeni kuhusu ada elekezi katika shule binafsi MANYANYA amesema ada elekezi inatolewa kutokana na mahali shule ilipo na kuzingatia gharama zilizotumika katika miundombinu ya shule husika na serikali itaendelea kusimamia ada hizo  ili kuhakikisha hakuna unyanyasi wa ulipaji wa ada hizo
Naibu Waziri wa Elimu, sayansi, teknolojia na ufundi mhandisi STELLA MANYANYA ametolea ufafanuzi swali lililoulizwa na mbunge KAWE HALIMA MDEE kuhusu ada elekezi katika shule binafsi na kusema hata hivyo vikao vinaendelea kati ya serikali na wamiliki wa shule kwa ajili ya kuliweka sawa jambo hilo.

No comments:

Post a Comment