Wednesday 20 April 2016

Jitihada za kusaka mtandao wa wahalifu zafanikiwa mkoani TABORA

Kamanda wa polisi wa mkoa wa TABORA Kamishina msaidizi HAMISI ISSAH

Kamanda wa polisi wa mkoa wa TABORA Kamishina msaidizi HAMISI  ISSAH amesema kuwa jitahada za kuunasa  mtandao wa kundi la wahalifu wa kutumia silaha ambao  umekuwa. 
ukihusishwa na ujambazi katika maeneo mbalimbali mkoani humo zimepata mafanikio baada ya kuikamata silaha ambayo imekuwa ikitumika katika matukio ya ujambazi mkoani humo.
   Kamanda ISSAH ametoa kauli hiyo baada ya kukamatwa kwa silaha hiyo ya kivita na risasi zake 22 na magazine moja, tochi moja,makoti matatu na pikipiki moja iliyoporwa katika kijiji cha KIZEGI wilayani UYUI.
Kamanda ISSAH amesema vitu hivyo vimekamatwa kwenye msitu wa kijiji cha  UTYATYA wilayani SIKONGE ambapo ameongeza kuwa  Silaha hiyo inasemekana imetumika katika ujambazi katika wilaya za NZEGA, UYUI na SIKONGE.

No comments:

Post a Comment