Katibu
Mtendaji Mamlaka ya Leseni ZANZIBAR RASHID ALI SALUM amesema endapo
wajasiriamali wataweza kuzingatia uzalishaji wa ubora wa bidhaa basi
kunauwezekano mkubwa wa kupata masoko ya uhakika nje ya nchi
Akizungumza na wajasiriamali katika semina mjini Unguja inayohusu masuala ya kuboresha bidhaa katika kiwango cha kimataifaAmesema licha ya kuweko kwa changamoto za uzalishaji wa ubora wa bidhaa lakini bado kunahaja ya kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinakidhi mahitaji ya ndani na nje ya nchi
Naye Kaimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Maendeleo ya Viwanda UNIDO GERALD RUNYORO amesema katika ushindani huo wa kibiashara wajasiriamali wanapaswa kuzingatia ubora na ufungaji uwe katika muonekano mzuri na kuzingatia sheria za usajili wa bidhaa.
Semina hiyo imejumuisha wajasiriamali wa bidhaa za usindikaji, za kutengeneza kwa mikono, biashara ndogondogo na utalii kutoka Unguja na PEMBA.
No comments:
Post a Comment