Monday 18 April 2016

Madiwani Gairo wamkataa mkurugenzi

 

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Gairo.
 Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Gairo wamesema hawaridhishwi na utendaji kazi wa mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mbwana Magota kutokana na kutoitisha vikao halali vya madiwani na kushindwa kusimamia kwa usahihi fedha za miradi.


 Wakizungumza na Mwananchi Digital baada ya kuahirishwa kwa kikao maalum cha baraza la madiwani, madiwani hao walisema kuna miradi ya ujenzi barabara imetekelezwa katika kiwango duni na imeshaharibika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

 Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Rahel Nyangasi aliwaambia waandishi wa habari kuwa kwa muda mrefu wameomba kufanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika halmashauri hiyo lakini mkurugenzi hataki kuwapeleka.

 “Kikao cha leo tuliitisha wenyewe madiwani na agenda zilikuwa kujadili mustakabali wa halmashauri yetu kwani  mkurugenzi amekua haitishi vikao na tuna kero nyingi za wananchi za kujadili na hatujui tutazijadili wapi wakati hakuna vikao”
 Vikao ambavyo wanalalamikia madiwani hao ni vikao vya kamati za halmashauri ambavyo vinatakiwa kufanyika mara moja kila mwezi na kikao cha baraza la madiwani ambacho hufanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu.

 Wakati akiahirisha mkutano huo Mwenyekiti huyo aliwaambia madiwani kuwa wamekiuka taratibu za kuitisha kikao kwani kabla ya kikao hicho walitakiwa watume barua kwa mkurugenzi ya kuitisha kikao ikiwa imesainiwa na theluthi moja ya madiwani wote jambo ambalo halikufanyika.

No comments:

Post a Comment