Sunday 17 April 2016

Takwimu za Fistula Moro zamtisha makamu wa rais

 Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan
Makamu wa rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ameshtushwa na takwimu kubwa ya wakina mama wanaopatwa na ugonjwa wa Fistula mkoani Morogoro na hivyo kuwaagiza wataalamu wa afya ya uzazi kutoa elimu ya Fistula na uzazi salama.


Mama Samia amesema hayo baada ya kupokea taarifa ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Morogoro Dk, Ritha Lyamuya iliyoonesha kuwepo kwa wagonjwa 123 wa Fistula kwa mwaka ambao hufanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo ilionesha kuwa idadi hiyo kubwa ya wagonjwa wa Fistula inatokana na elimu ndogo kwa jamii kuhusu ugonjwa huo na pia hospitali hiyo inahudumia wananchi wa wilaya mbili ya Morogoro na manispaa ambapo hakuna hospitali ya wilaya.
 
Akizungumza na madaktari na wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Morogoro mara baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo makamu huyo wa rais alisema kuwa takwimu hiyo ni kubwa na lazima jitihada za kupunguza tatizo hilo zifanyike ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa akina mama wajawazito na jamii kwa ujumbe.

No comments:

Post a Comment