Sunday 17 April 2016

Makonda atoa tahadhari juu ya Athari za mvua zinazoendelea jijini Dar es salaam

makonda 
 Mvua zinazoendelea kunyesha jijini dsm kuanzia jana usiku zimesababisha maeneo mengi ya jiji hilo hususan makazi ya watu kukumbwa na mafuriko na kusababisha baadhi ya wakazi wa jiji hilo kuzikimbia nyumba zao.


Katika maeneo ya Temeke, Jangwani, Kunduchi pamoja na maeneo ya mabondeni hali imekuwa tete kutokana na nyumba kujaa maji huku baadhi ya wakazi wa nyumba hizo wakiwa katika juhudi za kuokoa mali zao.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana ametembelea katika baadhi ya maeneo ya jiji na kuwataka wakazi wake kuchukua tahadhari kutokana na mafuriko hayo huku pia akiwataka wale wote walioziba njia za kupita maji, mifereji kuzifungua mara moja ili kuepusha maafa zaidi kwa watu wengine.

Aidha katika barabara ya Bagamoyo eneo la Mbezi tanki bovu hali ilikuwa mbaya kutokana na mafuriko kukatiza barabara na kulazimisha magari kushindwa kupita eneo hilo na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo

No comments:

Post a Comment