Wednesday 27 April 2016

Mama Maria Nyerere Asante Rais Magufuli.

Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere leo amefanya ziara ya kutembelea daraja la Kigamboni ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema liitwe daraja la Nyerere kutokana na mchango wake wa kuunganisha watu.

Akizungumza katika ziara hiyo Mama Maria amesema kwamba daraja la Kigamboni lilikuwa lipewe jina la Rais Magufuli lakini Rais Magufuli akaamua lipewe jina la Nyerere kutokana na mchango wake kwa taifa jambo ambalo litawafanya watu wakumbuke walipotoka.

''Ninamshukuru sana Rais Magufuli maana lilikuwa lipewe jina lake lakini Mungu akamjalia akasema hapana tukumbuke tulipotoka, kwa hiyo najisikia vizuri sana na familia inajisikia vizuri sana''- Amesema Mama Maria.

Katika Ziara hiyo Mama Maria ambaye ameambatana na mwanaye ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki Makongoro Nyerere pamoja na msaidizi wa Mama Maria.

Daraja la Kigamboni ambalo lilizinduliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli lina urefu wa mita 680 ambapo ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Dar es salaam ambao hulazimika kuvuka bahari kwenda kigamboni au kutoka kigamboni kuja katikati ya jiji.

No comments:

Post a Comment