Wednesday 27 April 2016

Maamuzi ya mahakama kuhusu kesi ya Kamishna mkuu wa TRA haya hapa

Aliye kuwa Kamishna kuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Harry Kitilya , na waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya Stanbic Sioi Sumari na shose Sinare wamefutiwa shitaka la nane (8) la kutakatisha fedha na kubaki na mashtaka 7 katika kesi inayowakabili

Hata hivyo washitakiwa hao wamekwama kwa mara nyingine tena kupewa dhamana na kurudishwa rumande baada ya upande wa jamhuri kuwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufutiwa shitaka la nane (8) la utakatishaji fedha.

Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 29/4/2016  ambapo itasikilizwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Emirius Mcharo na mwendesha mashtaka mwandamizi wa serikali Herman Tibabyekomia.

No comments:

Post a Comment