Wednesday 27 April 2016

THERIA:Wataalam wa utunzaji wa Taarifa ni tatizo hospitali nyingi nchini

Chama cha Maafisa kumbukumbu na taarifa za afya nchini Tanzania (THERIA) kimesema kuwa Hospitali nyingi nchini zinakumbana na tatizo la kukosa taarifa sahihi za afya hali
inayopelekea matatizo makubwa katika kupanga bajeti za afya na kusababisha upungufu wa vifaa tiba, watumishi,na madawa.
Akiongea wakati wa kufungua Mkutano uliowakutanisha maafisa kumbukumbu nchini Mkuu wa kitengo cha utunzaji kumbukumbu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw Geofrey Semu amesema kuwa kila Hospitali inahitaji mwanataaluma anayejua kuandaa taarifa za afya kwa ufasaha kwani taarifa sahihi za afya ndizo zinazopelekea huduma sahihi za afya.

Aidha serikali itakuwa na uwezo wa kupanga bajeti zake katika sekta ya afya kama itakuwa na takwimu sahihi za mahitaji muhimu ya sekta hiyo hivyo ni vizuri kuhakikisha inazalisha maafisa kumbukumbu wa kutosha watakaoweza kuandaa takwimu stahiki.
Kwa upande wake Afisa mwandamizi wa utunzaji kumbukumbu wa Hospitali ya Muhimbili Rehema Mwaipaya amesema kuwa waajiri wengi wanaajiri watunza kumbukumbu ambao hawana taaluma katika sekta ya afya hali inayowawia ugumu kujua mambo ya msingi ya kufanya katika kutunza kumbukumbu za mambo yahusuyo afya.

No comments:

Post a Comment