Wednesday 27 April 2016

Mapya yaibuka Jijini Dar es salaam UDA na Machinga Complex kurudishwa

Sakata la wamiliki wa Makampuni yanayo simamia uendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi unazidi kuibuwa mapya mara baada ya halmashauri ya jiji kukana kutambua kampuni ya Simon Group ambao wanadai kuwa na ubia katika mradi huo.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wa Meya wa jijini la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita, Mjumbe wa Baraza la Halmashauri kuu ya jiji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ubungo Mhe. Said kubenea amesema Halmashauri ya jiji haijauza hisa zake kwa Simon Group na kumtaka mmiliki wa Kamapuni hiyo kukimbilia Mahakami kwani mchakato wake haukuwa halali.

Mhe. Kubenea amesema ni vyema Serikali ikaingilia kati kuondoa utata huo ambao usiposhugulikiwa mapema utaligarimu taifa kutokana na kampuni ya Simon Group kukopa fedha nyingi katika taasisi za kifedha hapa nchini kwa ajili ya kuendesha mradi huo ambao usipofanikiwa utaangusha uchumi wa taifa.

Aidha kubenea ameiomba serikali kuu kuingilia kati sakala hilo ambalo linazidi kuwa na sintofahamau baada ya mchakato wake kugubikwa na udanganyifu mwingi ambao unalipotezea taifa mabilioni ya fedha nakwamba mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti ya CAG izingatiwe.

Naye Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amesema mchakato wa kurudisha vitega uchumi vya mapato ya jiji umefika na kuwa ameunda kamati mbili kuchunguza mradi wa machinga Coplex, kuhakiki makusanyo katika soko la kariakoo, UDA, ikiwa pamoja na kuongeza makusanyo ja jiji kutoka Bilioni 11.7 mpaka bilioni 20 kwa mwaka.

Akiongelea kamati hizo Meya amesema, maeneo muhimu yatakayo angaliwa nipamoja na makusanyo katika soko la Kariakoo, Maduka yanayozunguka eneo la shuke ya Benjamin Mkapa,Machinga Complex, shirika la usafiri la Dar es salaam UDA.

Aidha meya amesema watatumia Bilioni 4 kumaliza kabisa tatizo la Madawati katika shule za jiji la Dar es salaam, na kukarabati barabara ili wananchi wasilalamikie huduma za kijamii sambamba na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano katika ulipaji kodi

No comments:

Post a Comment