Friday 29 April 2016

Masalio yenye miaka takriban 550 yapatikana pwani ya Tanzania Tazama hapa

 
Mpiga mbizi mmoja anaamini amegundua kile ambacho huenda ni mji mkongwe kutoka pwani ya Tanzania ambao ulimezwa na bahari, kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la nchini humo Dar Post.

Eneo lililogundulika
Katika blogu yake Alan Sutton amesema alikuwa kwenye helikopta akielekea kisiwa cha Maffia wakati 'aliona muundo fulani ndani maji'.

Alirudi katika sehemu hiyo na kugundua masalio yenye umbali wa kilomita 3.5
Amekadiria kwamba huenda masalio hayo yana miaka takriban 550.
Hii ni kutokana na kuta za matumbawe - ambazo zina upana wa mita 2.5 na anasema kwa kawaida matumbawe hukuwa kwa milimita 4.5 kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment