Mashindano ya kimataifa ya Riadha ya kikanda ya vijana
chini ya miaka 20 yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Makamu
wa kwanza wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania RT Wiliam Kalage
amesema, nchi shiriki 11 za michuano hiyo zimeshawasili pamoja na
viongozi zikiwa tayari kwa ajili ya mashindano hayo yatakayofikia tamati
Aprili 30 mwaka huu siku ya jumamosi.
Kalage amesema, timu zote shiriki zimefikia eneo maalumu ambalo ni
kijiji cha michezo kilicho andaliwa kwa ajili ya mashindano hayo huku
ratiba rasmi ya ufunguzi wa mashindano hayo ikitarajiwa kutatolewa hapo
kesho mchana.
Nchi shiriki za mashindano hayo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Elitrea,
Sudan, Ethiopia, Sudan Kusini, Zanzibar, Djibout na Tanzania ambaye ni
mwenyeji wa mashindano hayo
No comments:
Post a Comment