Mkuu
wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ( kushoto ) akiwa na makamanda
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) katika mapokezi ya mwili wa
Brig General (Mstaafu) Ernest Galinoma nyumbani kwake Kalenga.
Jana
tarehe 20/04/2016 usiku Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela
aliongoza waombolezi katika mapokezi ya mwili wa Brig General (Mstaafu)
Ernest Galinoma nyumbani kwake Kalenga.
Marehemu alifariki juzi jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kalenga.
Shughuli za ibada zitaanza saa 6 mchana katika kanisa katoliki Kalenga. Bwana ametoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
Makamanda
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) wakiteremsha mwili wa Brig
General (Mstaafu) Ernest Galinoma baada ya kuwasili nyumbani kwake
Kalenga.
Makamanda
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) wakiwa wamebeba jeneza lenye
mwili wa Brig General (Mstaafu) Ernest Galinoma kuuingiza nyumbani
kwake Kalenga.
No comments:
Post a Comment