Wednesday 20 April 2016

Majipu ya tumbuliwa ilala jijini Dar es salaam Wahandisi 4 wasimamishwa kazi

 
Katika Kuunga Mkono falsafa ya Dr.John Magufuri ya Kutumbua majipu na Kuwashughulikia watumishi wasio waadilifu pamoja na wale wanaotumia Vibaya madaraka waliyopewa halmashauri ya manispaa ya Ilala 

 imewewasimamisha kazi wahandisi wanne waliokuwa wakisimia miradi ya barabara ya manispaa hiyo wakiongozwa na mkuu wa Idara ya uhandisi Injinia Jaffar Bwigane.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm Mstahiki meya wa manispaa ya Ilala Charles Kuyeko amesema wakuu hao wa idara ya uhandisi ambao walikuwa wakisimamia ujenzi wa barabara hizo wamekuwa wakilalamikiwa kwa muda mrefu kutokana na Usimamizi duni wa miradi ya barabara ya manispaa hizo ambazo asilimia 98 zimejengwa chini ya kiwango.
Amesema kusimamishwa kwa watumishi hao kutaenda sambamba na Uchunguzi wa kuchunguza ni kiasi gani cha hasara kilichosababishwa lakini pia hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya wahusika akiwepo Injinia Daniel Kirigiti na Siajali Mahili .
Aidha Meya huyo amesema barabara zote zilizojengwa chini ya kiwango na kuharibika katika kipindi kifupi wakandarasi waliopewa kazi hiyo watawajibika kuzitengeneza kwa kutumia Fedha zao.
Akizungumzia Suala la kuzagaa kwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga bw,Kuyeko amesema wameandaa mpango makakati wa kutenga maeneo maalum ili wafanyabiashara hao wafanye biashara zao bila kusababisha msongamano katikati ya maeneo ya Kariakoo.

No comments:

Post a Comment