Benki
ya NMB imesaini mkataba wa makubaliano na taasisi ya kutoa mikopo kwa
huduma za afya ya Uholanzi - MCF ili kudhamini kampuni ndogo za watoa
huduma za afya, hospitali na maduka ya dawa binafsi kujipatia mikopo ya
kati ya shilingi milioni 30 na bilioni mbili.
Wakizungumza wakati wa utilianaji saini mkataba huo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, INEKE BUSSEMAKER na Afisa Mtendaji Mkuu wa MCF, MONIQUE DOLFING-VOGELENZANG wamesema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka ambapo utaongeza utoaji wa huduma za kiafya katika maeneo mengi.
Naye Afisa wa huduma za kibenki kwa wateja wadogo wa NMB ABDULMAJID NSEKELA amesema mikopo hiyo itawalenga zaidi wamiliki wa hospitali na maduka ya dawa binafsi ambao wanahitaji mitaji ya kukuza biashara zao.
No comments:
Post a Comment