Friday 15 April 2016

Wawili wasimamishwa kazi kwa kusababisha hasara ya mamilioni

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. STEVEN KEBWE amewasimamisha kazi maafisa wawili wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro na kuagiza kukamatwa watu watatu wakiwemo raia wawili kutoka CHINA
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe, (katikati) pamoja na ujumbe wake wakifanya ukaguzi wa kushitukiza
Mkuu wa mkoa wa Morogoro  Dkt. STEVEN KEBWE amewasimamisha kazi maafisa wawili wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro na kuagiza kukamatwa  watu watatu wakiwemo raia wawili kutoka CHINA wa Mgodi wa mawe ya kutengenezea marumaru cha ZHAN FA CONSTRUCTION MATERIAL GROUP kwa tuhuma za kuisababishia Halmashauri hiyo hasara ya shilingi milioni  92 kwa kukwepa kodi.

Akitoa maagizo hayo mbele ya Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Dkt.  KEBWE amesema amefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa  kiwanda hicho kilikuwa kimefungiwa na serikali tangu  mwaka 2010 lakini kikakiuka agizo hilo  na kuendelea  na  uzalishaji huku  maafisa hao wa Halmashauri wakishindwa kufuatilia mapato ya Halmashauri kwa kipindi cha miaka sita mfululizo.

Waliokamatwa kujihusisha kuendesha mgodi huo kinyume cha sheria ni pamoja na  SHIQING  LIANG ,WANG JUN  na HILARY PAUL wote wakiwa ni  wafanya kazi  wa mgodi huo.

Dkt. Kebwe pia ametembelea baadhi ya maeneo ya mgodi huo na kubaini shughuli nyingine za usafishaji wa dhahabu kinyume cha taratibu ambapo pia amekuta viroba vilivyofungashwa mchanga  wa dhahabu.

No comments:

Post a Comment