Tuesday, 19 April 2016

Sehemu ya yaliojili Bungeni leo haya hapa











 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira JANUARY MAKAMBA
 
Matumizi ya mifuko wa plstiki mwisho june 2016
Serikali imetangaza kuwa itapiga marufuku uzalishaji na matumizi ya Mifuko ya aina zote za Plastiki kuanzia Julai mosi mwakani, 2017
Kauli hiyo imetolewa Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira JANUARY MAKAMBA wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni Dodoma.
Awali, Naibu Waziri LUHAGA JOELSON MPINA aliliambia Bunge kuwa Serikali imeamua kufanya hivyo na kwamba Kanuni za uzuiaji, Uzalishaji, Uagizaji, Ununuzi na matumizi ya Mifuko hiyo imeshapitishwa tangu mwaka 2006.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi HAMAD YUSUF MASAUNI ameliambia Bunge kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi, UNHCR ipo katika hatua za mwisho kufanya uhakiki kamili wa Wakimbizi ili kutoa Uraia kwa wanaostahili.

Naye  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dr MEDARD KALEMANI amewatoa hofu Watanzania kuwa pamoja na Wafadhili ikiwemo Serikali ya Marekani kujitoa katika kufadhili Miradi ya Changamoto za Milenia, MCC awamu ya tatu, Ujenzi wa Miradi hiyo ikiwemo usambazaji wa Umeme itaendelea kwa kutumia uwezo wa ndani.

No comments:

Post a Comment