Friday 15 April 2016

Serikali yapiga marufuku benki kukopesha kwa dhamana ya ofa ya viwanja


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI amepiga marufuku benki zote nchini kutoa mikopo kwa kutumia dhamana ya viwanja vyenye ofa
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali, kushoto ni Bibi Medelina Kiwayo Meneja Usimamizi wa Taasisi za Fedha-Benki Kuu na Tuse Joune Kaimu Mkurugenzi Mkuu Chama cha Wenye Mabenki Tanzania (TBA).
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI amepiga marufuku benki zote nchini kutoa mikopo kwa kutumia dhamana ya viwanja vyenye ofa badala yake amewataka watumie viwanja vyenye hati.

Waziri LUKUVI ametoa kauli hiyo jijini DAR ES SALAAM alipokutana na kufanya mazungumzo na jumuiya ya wenye mabenki nchini kujadili jinsi watakavyochangia kuongeza kasi ya watanzania kupimiwa viwanja na utatuzi wa changamoto mbalimbali zilizo kwenye sekta ya ukopeshaji kupitia ardhi.

Halikadhalika Waziri LUKUVI amezitaka benki kuhakikisha zinakua na mfumo wa ufuatiliaji wateja wanaokopa fedha kwa ajili ya miradi ya kilimo ili kujiridhisha kama fedha hizo zimetumika kama zilivyoombwa ama vinginevyo.

No comments:

Post a Comment