Friday 15 April 2016

TAKUKURU yabaini watumishi hewa watano Mwanza

Wakati Halmashauri ya jiji la Mwanza ikidai kuwa haina watumishi hewa bali watumishi watoro wapatao 60, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha Mkoani Mwanza Mhandisi HENRY MAKALE, leo akitoa taarifa ya Utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa Wanahabari 
 
Wakati Halmashauri ya jiji la MWANZA ikidai kuwa haina watumishi hewa bali watumishi watoro wapatao 60, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini-TAKUKURU mkoa wa MWANZA imebaini kuwepo kwa watumishi hewa watano ambao majina yao hayakuwasilishwa kwa mkuu wa mkoa huo JOHN MONGELLA.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa MWANZA, HENRY MAKALE amesema taasisi hiyo inaendelea na uchunguzi wa sakata hilo na utakapokamilika Mkurugenzi pamoja na Afisa Utumishi wa jiji la MWANZA watachukuliwa hatua za kisheria kwa kushindwa kuwasilisha majina ya watumishi hao ambao ni hewa.

Kamanda MAKALE ametumia fursa hiyo kueleza taarifa ya utendaji kazi ya taasisi hiyo ambapo katika kipindi cha januari hadi machi mwaka huu imepokea malalamiko  27 kuhusu vitendo vya rushwa.

Idara zinazolalamikiwa ni pamoja na ardhi, mahakama, polisi na afya.

Katika kipindi hicho pia TAKUKURU mkoa wa MWANZA imewafikisha mahakamani watuhumiwa TISA akiwemo aliyekuwa Meya wa Manispaa ya ILEMELA, HENRY MATATA.

No comments:

Post a Comment