Friday 15 April 2016

Sudan Kusini yasaini mkataba kuingia EAC

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki –EAC, Rais JOHN MAGUFULI na Rais SALVA KIIR wa SUDAN KUSINI wametiliana saini mkataba wa SUDAN KUSINI kuingia rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki CEAC) na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir wakibadilishana hati za makubaliano ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kusaini
Utiaji saini huo umefanyika jijini DAR ES SALAAM baada ya Rais SALVA KIIR wa SUDAN KUSINI kuwasili nchini mapema leo.

Mwezi uliopita, viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki waliidhinisha kukubaliwa kwa SUDAN KUSINI kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano wa wakuu wa nchi hizo zinaounda Jumuiya hiyo uliofanyika mjini ARUSHA.

SUDAN KUSINI inakuwa nchi ya SITA kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Baada ya kujiunga rasmi leo, SUDAN KUSINI inatarajiwa kufungua mipaka yake kwa ajili ya biashara.

No comments:

Post a Comment