Walioapishwa ni LUCY OWENYA, OLIVER SEMUGURUKA, RITHA KABATI na SHAMSI VUAI NAHODHA.
Katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, HAMAD YUSUF MASAUNI ameliambia bunge kuwa serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi - UNHCR ipo katika hatua za mwisho za kuhakiki idadi kamili wa wakimbizi ili kutoa Uraia kwa wanaostahili kama Rais alivyoahidi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dokta MEDARD KALEMANI amewatoa hofu watanzania kuwa pamoja na Shirika la Changamoto za Milenia -MCC kujitoa katika ufadhili katika ya Awamu ya TATU, ujenzi wa miradi iliyokuwa ikifadhiliwa na MCC ikiwemo usambazaji wa umeme itaendelea kwa kutumia uwezo wa ndani.
No comments:
Post a Comment