Wakazi
wa Jiji la TANGA wamewaomba wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania kuondoa tofauti zao za vyama pindi wawapo bungeni lengo likiwa
ni kujadili
Wakazi wa Jiji la TANGA wamewaomba wabunge wa Bunge la
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuondoa tofauti zao za vyama pindi
wawapo bungeni lengo likiwa ni kujadili miswada kwa ufasaha na kuwaletea
maendeleo wananchi.Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kipindi cha uchaguzi kimekwishapita kwa sasa kinachotakiwa ni kuungana na kuwasaidia wananchi pamoja na taifa zima ili kufikia malengo yaliokusudiwa.
Wamesema iwapo wabunge wote wataungana ni dhahiri kuwa kasi nzuri ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya TANO itafikia malengo yake kwa haraka.
Aidha wameongeza kuwa swala la baadhi ya wabunge kutoka nje wakati vikao vya bunge vikiendelea ni swala linalowanyima haki wananchi wa maeneo waliyotoka wabunge kwa kuwa wanapoteza muda wa kuchangia hoja za majimbo yao
No comments:
Post a Comment