Thursday, 21 April 2016

Wafanyakazi Waliomaliza muda wa kazi nje ya nchi sasa kurudishwa

Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,Wizara ya Mambo ya nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Bi Mindi Kasiga akizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, wa wizara hiyo Bi Mindi Kasiga amesema miongoni mwa watumishi watakaorejea nchini wamo mabalozi, maafisa, wahasibu na makatibu muhtasi.
Wizara hiyo imejipanga kuwapeleka kwenye balozi zake nje watumishi wapatao 105 na kuwarejesha nchini wengine 79 ambao miongoni mwao muda wao wa utumishi katika balozi hizo umemalizika na wengine kustaafu kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.
Wakati huohuo wizara imetolea maelezo ya ziara ya kikazi nchini Tanzania ya waziri wa Viwanda na Biashara wa Oman Mheshimiwa Dkt Ali Bin Masoud Al Sunaidy katika ziara hiyo waziri Al Sunaidy aliongozana na ujumbe wa watu 108 ambapo 12 walikuwa ni maafisa toka taasisi mbalimbali katika serikali ya Oman na wengine waliobakia toka sekta binafsi ndani ya nchi hiyo kwa lengo la kukutana na taasisi kama hizo nchini.

No comments:

Post a Comment