Tuesday 26 April 2016

Watuhumiwa 96 wakamatwa na Jeshi la polisi jijini Dar es salaam.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, - SIMON SIRRO amesema  kuwa kati ya watuhumiwa hao 86 wamekamatwa  kwenye maeneo ya UKONGA, KIJITONYAMA, MAGOMENI, na OSTERBAY.

Katika hatua nyingine Kamishna SIRRO amesema mnamo tarehe 23 APRIL mwaka huu jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata jumla ya majambazi KUMI na Watatu  ikiwa ni mwendelezo wa kuwatafuta majambazi waliohusika katika tukio la wizi kwenye benki ya ACCESS TAWI  Mbagala Jijini DSM tarehe 26 February mwaka huu

No comments:

Post a Comment