Monday, 25 April 2016

Yanga kufanya uchaguzi June 05 mwaka huu

Timu ya Soka ya Yanga FC yenye maskani yake Jijini Dar es Salaam inatarajia kufanya uchaguzi wake Juni 5 Mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) Aloyce Komba amesema, uchaguzi Yanga utasimamiwa na kamati ya uchaguzi ya TFF kutokana na klabu hiyo kuwa na viongozi ambao wameshamaliza muda wao huku kamati ya uchaguzi ndani ya klabu hiyo ikiwa imezuiwa kuchukua jukumu hilo.
Kombe amesema, ikifikia Mei tatu kamati hiyo itatangaza kila kitu kuhusu uchaguzi huo ikiwemoKkatiba itakayotumika katika uchaguzi huo pamoja na nafasi za wagombea ndani ya klabu hiyo.

Yanga inaanza mchakato wake wa uchaguzi baada ya Baraza la Michezo nchini (BMT) kutoa agizo kwa klabu hiyo kuhakikisha imefanya uchaguzi wake mpaka ifikapo mwishoni mwa mwezi June mwaka huu.

No comments:

Post a Comment